KCPE 2006 KISWAHILI

KENYA NATIONAL EXAMINATION COUNCIL

35271-KCPE 2006

KISWAHILI

PAPER


 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi

umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kandamiza hakujua thamani ___1___ watoto ___2___ siku moja ___3___ na ulimwengu. Alizoea

kuwatumikisha watoto wadogo kwa ___4___ kuwaajiri watu wazima asije akajiumiza kwa kuwalipa

mishahara mikubwa. Siku moja mwanawe mmoja ambaye ___5___ kuyamudu masomo aliamua kuondoka

nyumbani bila kuaga. Kandamiza alipogundua kuwa mwanawe ___6___ mjini aluhuzunika mno. Moyoni

Kandamiza alijua kuwa mtoto huyo ___7___ jinsi yeye alivyowafanya watoto wa wengine.

A B C D

 1. Wa la za ya
 2. Sasa hadi tangu lau
 3. Alipofunzwa alikofunzwa aliofunzwa aliyefunzwa
 4. Kuchelewa kupenda kucheka kupendelea
 5. Hawezi hakuweza hataweza hajaweza
 6. Ametoroka ametoroshwa ametorokea ametorosha
 7. Angetesa angemtesa angewatesa angeteswa

Taifa lolote___8___ wananchi wenye afya. Magonjwa ___9___ nchi hasara ___10___ pia huwa

mzigo mzito kwa mtu binafsi. ___12___ ya magonjwa hutokana na___13___usafi. ___14___

huweza kuzuiwa iwapo wananchi wataitikia wito wa kunadhifisha makazi ___15___

A B C D

 1. Huhitaji hahitaji yahitaji lihitaji
 2. Hailetei haileti hayaleti hayailetei
 3. Ajabu kamwe tu naam
 4. Bali mbali na ijapokuwa
 5. Baina baadhi kati zaidi
 6. Kutodumisha kutodumu kudumisha kudumu
 7. Hii hizi hiyo haya
 8. Lao yao zao wao

 

 

 

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30 chagua jibu lililo

sahihi

 1. “Ki” imetumiwaje katika sentensi: Mweni

alipokuja alinipata nikifyeka

 1. Kuonyesha hali ya masharti
 2. Kuonyesha hali ya kukanusha
 3. Kuonyesha hali ya kuendelea
 4. Kuonyesha hali ya udogo
 5. Ni sentensi ipi sahihi?
 6. Ndizi lililoletwa ni langu
 7. Miti zilizopandwa zimeota
 8. Zulia iliyonunuliwa ni zuri
 9. Wema unaozungumziwa ni huu
 10. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili, ni sehemu

ipi iliyo tofauti na zingine?

 1. Paja
 2. Kiganja
 3. Pafu
 4. Goti
 5. Polepole, vibaya, alasiri, njiani, ni
 6. Vielezi
 7. Vivumishi
 8. Nomino
 9. Viwakilishi
 10. Methali inayotoa funzo kuwa: jambo

linaloonekana zito kwa mwingine laweza kuwa

rahisi kwako ni;

 1. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
 2. Mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi
 3. Kila mwamba ngoma ngozi huvutia kwake
 4. Ganda la muwa la jana chungu kaona

kivuno

 1. Sentensi “Asingalikwenda kwake asubuhi

ansingalimkuta” ina maana kuwa;

 1. Hakuenda kwake asubuhi lakini alimkuta
 2. Alienda kwake asubuhi lakini hakumkuta
 3. Alienda kwake asubuhi na akamkuta
 4. Hakuenda kwake asubuhi wala hakumkuta
 5. Ni maneno yapi ambayo yote ni viunganishi?
 6. Ila, ingawa, lakini, maadamu
 7. Huyu, hao, ovyo, na
 8. Ila, lakini, vizuri, wima
 9. Ingawa, isipokuwa, zuri, safi
 10. Kivumishi cha sifa kutokana na kitenzi angaa ni:
 11. Angaza
 12. Angazia
 13. Angavu
 14. Angalau
 15. kwa maneno ni:
 16. Subui nane
 17. Thumuni saba
 18. Subui
 19. Thumuni
 20. Kisawe cha neno barobaro ni
 21. Banati
 22. Kijana
 23. Mvulana
 24. Shaibu
 25. Nomino habari iko katika ngeli ya:
 26. U-ZI
 27. I-I
 28. U-I
 29. I-ZI
 30. Tano ni kwa chokaa. Kitita ni kwa
 31. Pesa
 32. Funguo
 33. Ndizi
 34. Ngozi
 35. Haya ni maumbo gani?

 

 

 1. Pembe tatu, Mche, Duara
 2. Pia, Mcheduara, Nusuduara
 3. Pia, Mchemramba, Mcheduara
 4. Pembe tatu, Pia, Nusuduara
 5. Chagua usemi halisi ufaao wa:

Bahati alisema kuwa angeenda nyumbani

kupumzika

 1. “Nimeenda nyumbani kupumzika,” Bahati

alisema

 1. “Niende nyumbani kupumzika,” Bahati

alisema

 1. “Nitaenda nyumbani kupumzika,” Bahati

alisema

 1. “Nilienda nyumbani kupumzika,” Bahati

alisema

 1. Yapange maneno yafuatayo kulingana na jinsi

yanavyotokea katika kamusi:

(i) Bandika

(ii) Beua

(iii) Birika

(iv) Baidika

 1. (i) (iv) (ii) (iii)
 2. (iv) (ii) (iii) (i)
 3. (ii) (i) (iii) (iv)
 4. (iv) (i) (ii) (iii)


 

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 31 mpaka 40

Huko Tujueni aliishi mtu kwa jina Mkazeni. Mkazeni alikuwa maarufu katika kutabiri ndoto. Alijulikana

pia kwa kuyadadisi mambo yaliyozuka humo kijijini mwao. Kwake kulifurika watu ambao aliwahudumua

bila malipo.

Wakati fulani Mkazeni alioteshwa kuwa kulikuwa na magari na matrela ambayo yalikuwa

yakisimamishwa humo kijijini. Madereva wake walikuwa watu waliojaa wadudu tele mwilini. Madereva hao

walikuwa wakiwalaghai vijana kijijini huku wakiwaachia “zawadi” zilizileta “vilio”. Alipowaeleza wanakijiji

wakamcheka na kumwambia, “sasa nguvu zako za utabiri zinapotea . utawezaje kufikiria kuwa magari hayo

yataleta balaa? Magari hubebea mali!”

Ingawa maneno hayo yalisemwa kiutaniutani, yalimchoma maini, akaamua kufyata ulimi na kukaza nia

yake. Alijitahidi kuihimiza aila yake kuhusu umuhimu wa tabia njema.

Siku nyingine tena akaota ndoto kuwa huko Tujueni kumeingia joka kubwa lililowameza vijana

wengi.Ingawa wanakijiji walikuwa wamepuuza hapo awali; aliwafafanulia ndoto hiyo nao wakazidi

kumcheka. “Sasa tena utabiri umeleta mambo ya nyoka? Tangu uzaliwe umewahi kumwona nyoka kama

huyo?” hapo Mkazeni akaona amedharauliwa kupita kiasi, akaamua “kujimezea” utabiri wake mwenyewe,

lake liwe jicho tu. Watu ambao waliamua kutojihadhari kabla ya hatari, angewafanya nini? Kidole kimoja

kingevunjaje chawa?

Miaka michache ikapita, nayo magari na matrela ya kikweli yakafika pale na kupafanya kituo cha

mapumziko. Madereva wakaiona sehemu hiyo ikiwa na starehe nyingi. Tujueni ikajulikana. Bishara

madukani na kwenye masoko zikaongezeka.

Baadhi ya watu waliokuwa wamepuuza Mkazeni wakasema, “Oneni mtabiri yule na ndoto zake. Maafa

aliyoyatabiri ni hizi pesa tunazozipata? Alitaka tufe maskini? Muone sasa, amenyamaza jii kama maji ya

mtungi. Anasema anaihubiria familia yake isijihusishe na biashara haramu. Biashara gani haramu hapa? Cha

kupata si cha kuiba.”

Baada ya muda, familia nyingi zikaanza kulia. Utabiri ukaja kutokea kweli. Wadudu walikuwa ni

UKIMWI na joka likawa maangamizi yaliyoletwa na madhara ya UKIMWIA. Wanakijiji waliathirika na

kujuta. Kituo hicho cha biashara kikawa na sifa mbaya. Watu wengi wakafa na biashara ikazidi kufifia.

Mkazeni akawa anasikitishwa na matokeo ya mapuuza na tamaa za wanadamu. Kwake yeye na familia

yake waliendelea kuishi vyema kinidhamu.

 1. Mkazeni alikuwa karimu kwa sababu
 2. Alitabiri mambo mengi bila chuki
 3. Aliwatabiria watu mambo bila kuwalipisha
 4. Watu wengi walimwendea kwa utabiri
 5. Watu wengi walimdharau lakini hakulipiza
 6. UKIMWI ndotoni unaweza kulinganishwa na
 7. Wadudu na joka kubwa
 8. Matrela na madereva
 9. Madereva wenye wadudu

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 1. Wanakijiji wanaposema, “Sasa nguvu zako za

utabiri zinapotea” wanamaanisha

 1. Mkazeni si mtabiri tena
 2. Wanaushuku utabiri wa mkazeni
 3. Hawautaki utabiri wa Mkazeni
 4. Mkazeni hutabiri yasiyo ya kweli
 5. Bishara madukani ziliongezeka kwa sababu
 6. Watu wengi walikuja kutafuta utabiri wa

Mkazeni

 1. Kulikuwa na starehe nyingi katika masoko
 2. Tujueni ilikuwa kituo cha mapumziko cha

madereva wa matrela

 1. Tujueni ilijulikana na madereva wa matrela

makubwa

 1. Watu wengi wa tujueni walikuwa ni
 2. Wenye tamaa na watabiri
 3. Wapuuzaji na watabiri
 4. Wenye tamaa na malezi bora
 5. Wapuuzaji na wenye tamaa
 6. Kulingana na taarifa hii, UKIMWI uliendelezwa

sana na:

 1. Madereva wa magari na matrela
 2. Wafanyibiashara wenye matrela na magari
 3. Madereva wapitiao katika vituo vya biashara
 4. Wazazi wenye tamaa ya kupata mali
 5. Baada ya Mkazeni kupuuzwa tena alichukua

hatua zipi?

 1. Alitabiri mara ya pili na kungojea matokeo
 2. Alibishana na wapuuzaji na kuwapa

matokeo

 1. Aliwaangalia tu waliompuuza na kuendelea

kutabiri

 1. Alinyamaza, akaongoza familia na kungoja

matokeo

 1. Kutojihadhari kabla ya hatari ni sawa na:
 2. Kutojitayarisha kukabiliana na tatizo
 3. Kutoshughulika na hatari
 4. Kutoshughulikia matatizo yajapo
 5. Kutoogopa madhara ya tatizo
 6. Familia ya Mkazeni ilinusurika kwa kuwa
 7. Ilikuwa ukufundishwa kuhusu utabiri
 8. Haikufanya biashara na madereva
 9. Ilizingatia maadili na mashauri
 10. Mkazeni alikuwa mtabiri
 11. Kichwa kifaacho zaidi kueleza kifungu hiki ni:
 12. Mkazeni wa Tujueni na utabiri wake
 13. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
 14. UKUMWI utaangamiza watu wengi
 15. Mchelea mwana kulia hulia mwenyewe

 

 

 

Soma taarifa hii kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Maendeleo ya nchi hutegemea mchango na juhudi za kila mwananchi. Hata hivyo, ni jambo la kusikitisha

kuona kuwa baadhi yetu tuna fikira zisizo za kizalendo kuwa wengine ndio wanaopasa kuiendeleza nchi.

 

Watu wa aina hii hutarajia serikali kuwafanyia hili na lile. Huwathubutu kujiuliza je, mimi nimeifanyia nini

nchi yangu?

Inafaa tukumbuke kwamba nchi ni kama chombo cha usafiri na kila mtu ana wajibu wa kuhakikisha

kwamba chombo hicho kimekwenda ipasavyo. Tunahitaji kuwa na bidii za mchwa za kujenga kichuguu.

Tuwe na umoja wa nyuki ambao, japo ni viumbe wadogo hudiriki kutengeneza asali ambayo huwafaa wao na

kuwalisha binadamu. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kuilisha jumuiya, sembuse sisi?

Mungu amemtunukia kila mmoja wetu vipawa anuwai. Ni juu yetu kuvitumia vipawa hivi kuinua uchumi

wa nchi. Tukujitahidi pamoja tutaweza kutatua matatizo mengi yanayoikumba nchi. Tukumbuke kwamba

kinga na kinga ndipo moto uwakapo. Wananchi katika nyanja mbalimbali hawana budi kuziimarisha nyanja

hizi ili kuinua hali zao za maisha. Mathalani, wakulima watumie njia za kisasa za ukulima ili kuzalisha mazao

mengi. Wakifanya hivyo, tutaweza kukabiliana na baa la njaa ambalo linawadhuru wananchi wengi.

Vijana nao wana jukumu lao kwa taifa. Wewe kama mwanafunzi, unaweza kuchangia maendeleo ya nchi

hii kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za shule. Ujibidiishe vilivyo, si katika masomo pekee, lakini

pia katika michezo. Kwa kuiendeleza michezo ya riadha na hata ya kuigiza, utakuwa umeiendeleza nchi kwa

kuukuza utamaduni wako. Isitoshe, unaweza kushiriki katika shughuli za kuzoa taka katika mtaa ulio karibu

na shule yako. Ukifanya hivyo utakuwa umeitikia wito wa serikali wa kuhufadhi mazingira.

Sehemu za mashambani zinahitaji kushughulikiwa kimaendeleo. Licha ya kuwa sehemu nyingi zina

rutuba, vijana wengi baada ya kupata masomo huhiari kuhamia mjini kutafuta kazi zenye hadhi. Mashamba

yameachiwa wazee na bila shaka mazao yamekuwa haba. Hebu tujiulize, je, ikiwa sisi vijana tutaziacha

sehemu zetu na kuhamia kwingine, nani atakayeziauni? Je, hatujui kuwa chetu ni chetu na nguo ya kuazima

haifai chochote? Ni vyema tukumbuke kuwa ikiwa tunataka kusaidiwa kuendeleza sehemu zetu, ni lazima sisi

wenyewe tuwe tayari kuzitumikia kwani abebwaye hujikaza. Mapenzi kwa nchi ni muhimu mno. Shime

tuungane kuijenga nchi yetu.

 

 1. Maendeleo ya nchi yanahitaji
 2. Kushughulikia kila mara katika kilimo
 3. Ushirikiano wa kila mwananchi
 4. Kutotarajia serikali kufanya lolote
 5. Watu wengine kuendeleza nchi

 

 1. Watu walio na fikra za kizalendo ni wale
 2. Wanaotarajia kusaidiwa kila mara
 3. Wanaowataka wengine kushughulikia

miradi ya maendeleo

 1. Wasiojua wameifanyia nini nchi
 2. Wasiopuuza wajibu wao katika kuendeleza

nchi

 

 1. Nchi ni kama chombo ch usafiri kwa sabau:
 2. Wananchi wasipoendeleza nchi itazorota
 3. Bila chombo usafiri haufanikiwi
 4. Wananchi wasiporudi mashambani nchi

itazorota

 1. Bila wasafiri nchi haifanikiwi

 

 1. Binadamu wanalinganishwa na nyuki kwani
 2. Wakiwa na bidii nyingi wanaweza kujifaidi

wao na wengine

 1. Nyuki wana umoja japo ni viumbe wadogo
 2. Wakiwa na umoja na bidii wanaweza

kujifaidi wao na wengine

 1. Nyuki na mchwa wana bidii za kujenga

 

 1. Katika kifungu, matendo yanayoonyesha ukweli

wa methali, “Kinga na Kinga ndipo moto

uwakapo” ni

 1. Vijana kuzoa taka na sote kushiriki katika

michezo

 1. Wote kurudi mashambani na kulima kwa

bidii

 1. Vijana kudumisha utamaduni na kuimarisha

elimu

 1. Ushirikiano wa nyuki na wananchi

kujitahidi pamoja

 1. Kulingana na kifungu, matatizo mengi

yatatatuliwa iwapo

 1. Tutafanya kazi kwa pamoja bila kuzingatia

tofauti zetu

 1. Sote tutakuwa na vipawa tofauti tofauti
 2. Sote tutajibidiisha katika masomo yetu
 3. Tutatarajia misaada kuinua hali za maisha

yetu

 1. Vijana
 2. Wanapaswa tu kushughulikia masomo
 3. Wanapaswa kusoma ili kukuza utamaduni
 4. Wanapaswa kushiriki kuiimarisha nchi

katika nyanja mbalimbali

 1. Wanapaswa kushirikiana wao kwa wao

kujiinua na kuimarisha kilimo

 1. Kulingana na kifungu maana ya kazi zenye

hadhi ni

 1. Kazi zinazolipa mishahara mikubwa
 2. Kazi zinazofikiriwa kuwa bora kuliko za

mashambani

 1. Kazi zenye marupurupu mengi kuliko za

mashambani

 1. Kazi za walio na elimu ya juu
 2. Kulingana na kifungu hiki, abebwaye hujikaza

ina maana

 1. Unaposaidiwa lazima nawe pia ujitahidi
 2. Ukibebwa mgongoni usilegee kamwe
 3. Tusitarajie kusaidiwa bila kusaidia
 4. Tukiwasaidia wengine lazima tujitahidi
 5. Ikiwa vidudu hivi vinaweza kulisha jumuiya,

sembuse sisi? Maana yake ni

 1. Nyuki wanaweza kulisha watu wengi
 2. Binadamu ana uwezo wa kushirikiana
 3. Nyuki wana ushirikiano kuliko binadamu
 4. Binadamu wana nguvu za kuzalisha kuliko

nyuki

You may also like...

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *